Je ni kweli
kuwa Mungu huwapatiliza wana DHAMBI za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha
nne?
Baadhi ya maandiko yanakubaliana na kauli
hii, kuwa dhambi za baba huamishiwa kwa watoto wao. Lakini ni vema tukatulia
kidogo na kuangalia uhalisia wa maneno haya, na maandiko mengine yanayotilia
msisitizo ama kukinzana na andiko hili.
Kwa upande mmoja inaonekana ni kweli Mungu
huwapatiliza wana maovu ya baba zao.
Kutoka 34:6-7
“BWANA
akapita mbele yake akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye
fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; wenye kuwaonea huruma
watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye
kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa
baba zao, na wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne”