Tolla G Tolla, kama raisi wa VOT alionesha maono ya kikundi hiki na kuamsha hamasa
miongoni mwa wajumbe waliohudhuria…wakiwa bado wachangaaaaa…waliimba baadhi ya
nyimbo zilizo kosha mioyo ya wengi na kuamsha mshawasha wa kuwasikia tena.

Leo ni miaka kama 2 sasa tangu kuanzishwa kwa kundi hili. Tayari
yamefanyika mengi na kukua kwa kundi hili kwaonekana bayana.
Siri kubwa ya mafanikio haya ni kule kujitoa pasi na mwisho
kwa waimbaji na wajumbe wa kikundi ndo kunako pelekea kuona maono yao ya mwaka 2010…..yakionekana
wazi.
Ni dhahiri kuwa Mungu anapotoa maono anayatoa kwa watu walio
tayari, kufanya, wapo waliokuwa mstari wa mbele lakini leo hawapo, wapo
walioona wakasadiki na kujiunga na wapo waliokuwa na imani wakaona yakitokea
wakiwepo. Sifa na SHUKRANI ZIMWENDEE MUNGU.
Ni ukweli kwamba wanamuziki wengi wa nyimbo za injili nchini
Tanzania hawana umoja huu ulioanza kwa VOT, hivyo mwamko huu uombewe na kupewa
msaada wa kifedha na kihali kufanya kazi ya
Bwana Yesu iende mbele.
Ni maombi yangu kuwa VOT wafanikiwe kila wakati….
No comments:
Post a Comment