Je ni kweli
kuwa Mungu huwapatiliza wana DHAMBI za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha
nne?
Baadhi ya maandiko yanakubaliana na kauli
hii, kuwa dhambi za baba huamishiwa kwa watoto wao. Lakini ni vema tukatulia
kidogo na kuangalia uhalisia wa maneno haya, na maandiko mengine yanayotilia
msisitizo ama kukinzana na andiko hili.
Kwa upande mmoja inaonekana ni kweli Mungu
huwapatiliza wana maovu ya baba zao.
Kutoka 34:6-7
“BWANA
akapita mbele yake akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye
fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; wenye kuwaonea huruma
watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye
kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa
baba zao, na wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne”
‘Usijifanyie
sanamu ya kuchong, mfono wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho
chini duniani , au kilicho majini chini ya nchi. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi
ni BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao;
hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu
wanipendao, na kuzishika amri zangu’
Walawi
26:39
“Na watu wa
kwenu watakaobaki watafifia kwa ajili ya uovu wao, katika hizo nchi za adui zenu; tne watafifia kwa ajili ya uovu wa baba zao, pamoja nawo"
Kwa upande
mwingine maandiko yanaonekana kukinzana na maandiko hayo mawili. Lakini sio kweli
kwamba yanakinzana.
Kumbukumbu 24:16
Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala
watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi
yake mwenyewe,”
2
Wafalme 14:6
Ila hakuwaua watoto wa hao wauaji; kama
ilivyoandikwa katika kitabu cha torati ya Musa, kama alivyoamuru BWANA,
akisema, mababa wasife kwa makosa ya wana , wala wana wasife kwa makosa ya
mababa; lakini kila mtu atakufa kwa kosa lake mwenyewe.“
Ezekia 18:20
“Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa;
mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe,
haki yake mwenye haki itakuwa juu yake na uovu wake menye uovu utakuwa juu
yake.”
Je maandiko
haya yanamahusiano gani?
Kwa jinsi Mungu alivyo na tabia zake haya
maandiko yanamahusiano makubwa. Kwanza; dhambi ya baba anaadhibiwa nayo mtoto
….hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao….kama wana hawajamjua Kristo
na kuunganishwa na agano la Kristo ni dhahiri kuwa dhambi za baba zao
zitaambatana nao.
Tabia moja wapo ya Mungu ni kuwa ni wa
haki…kwa mantiki hiyo Mungu huwaadhibu walio na makosa na sio wale waliotubia
makosa yao.
Pili; kwa sababu ya Kristo laana zote za aina
zote Yesu alizibeba msalabani . kwa mantiki hiyo kila aziungamae dhambi zake
kweli anasamehewa na anakuwa kiumbe kipya.
2 Kor 5: 17
Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo
amekuwa kumbe kipya; yakale yamepita tazama yamekuwa mapya”
1 Yoh 1:9
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu
na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
No comments:
Post a Comment